Msanii Diamond Plutnuz amewashangaza watu baada ya kauli yake kwamba
anaona bifu kwenye muziki na kitu kizuri, tofauti na wasanii wenzake
wengi ambao hupinga suala la bifu.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond amesema kwake
yeye anaona ni sawa tu iwapo wasanii wanakuwa na bifu, kwani inasaidia
kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wao, kwa kuzungumziwa na vyombo vya
habari na watu mbali mbali, isipokuwa inakuwa shubiri pale inapogusa
familia, na kutoleana maneno machafu.
“Bifu mi naona fresh, kwangu kitu kikizungumziwa ndo naona poa tu kwanza
inaniongezea, ila pale inapofikia kugusa kwenye familia na kutoleana
maneno machafu ndio inakuwa sio poa”, alisema Diamond Plutnumz.
Kutokana na kauli hiyo, Diamond amekuwa amepigia mstari kuwa wasanii wa
lebo yake ya WCB hutegemea ‘kiki’ zaidi kuliko kazi bora kuweza ku-hit,
kama ambvyo watu wengi huwatuhumu wasanii hao.
Pia Diamond ametoa siri kuwa mashabiki wake wajiandae mkao wa kula kwani
kabla mwaka huu kuisha, atatoa album ambayo itakuwa ya kimataifa.
Tuesday, August 9, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment