Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa baada ya
kuachana na mpenzi wake wa zamani Nay wa Mitego ambaye alimuweka wazi
kwa jamii na kuja kuachana baada ya muda mfupi alikuwa mwoga tena
kumuweka wazi mpenzi wake mpya.
Shamsa Ford alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ na kusema kuwa
alikuwa mwoga kumuweka wazi kwa jamii mpenzi wake mpya lakini kwa kuwa
mapenzi yamemzidi imebidi sasa amuweke wazi, kwani anasema mapenzi
huwezi kuyaficha.
“Mwanzo kweli nilikuwa naogopa lakini mapenzi yakizidi huna namna
inabidi tu ujiachie, ni kweli mpaka sasa tayari ameshanitolea mahari
nyumbani” alisema Shamsa Ford
Katika kusherehekea siku ya kuzaliwa Shamsa Ford alitumia nafasi hiyo
kumtambulisha mpenzi wake mpya ambaye anafahamika kwa jina la Chid
Mapenzi ambaye mara kadhaa alikuwa akisema ni mtu anayeshirikiana naye
kwenye biashara tu.
Wednesday, August 3, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment