Mtoto wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah Dangote
Agosti 3, mwaka huu ametimiza mwaka mmoja lakini jipya lililoibuka ni
kuhusiana na dawa ‘hirizi’ aliyovalishwa mkononi na bibi yake mzaa baba,
Sanura Kassim ‘Sandra’, Risasi limenyetishiwa ubuyu.
Chanzo kutoka ndani ya familia ya mastaa hao kilichoomba hifadhi ya jina
lake kimedai kuwa, awali Tiffah alivishwa dawa hiyo lengo likiwa ni
kumkinga na matatizo lakini Zari alipokwenda Sauzi akamvua kwa kuwa yeye
si ‘muumini’ wa mambo hayo.
tiffaIkadaiwa kuwa, baada ya Zari kumvua walikaa muda mrefu bila Tiffah
kuwa na ‘kadawa’ hako hali iliyomfanya mtoto huyo achelewe kutembea.
“Unajua ile dawa ina mambo mengi kwa watoto, inamsaidia kumkinga na
matatizo lakini pia inamfanya atembee haraka, sasa walipoivua ikamfanya
achelewe kutembea,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:
“Hali hiyo ilisababisha Zari na Diamond kutofautiana na mwisho
wakakubaliana hirizi irejeshwe mkononi mwa Tiffah ndipo mtoto huyo
alipoanza kutembea.”
Ikaelezwa kuwa, kuanza kutembea kwa Tiffah kumeibua furaha upya kwenye
familia hiyo kwani walishaanza kuwa na hofu hasa ikichukuliwa kuwa, Zari
ana mimba nyingine na anatarajiwa kujifungua Desemba, mwaka huu.
Kufuatia madai hayo, mwandishi wetu alimtafuta Diamond na alipopatikana
alisema kuwa ni kweli mtoto wao ameanza kutembea lakini si kwa sababu ya
dawa hiyo aliyofungwa mkononi.
“Hayo mambo ya kumvalisha na kumvua Tiffah ile dawa ya mkononi ni uamuzi
tu lakini huwezi kusema ina uhusiano na kutembea kwake,” alisema
Diamond.
Saturday, August 6, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment