Msanii wa muziki ambaye pia anafanya ‘modeling’ na utangazaji kwenye
Kituo cha Redio cha Choice FM cha jijini Dar, Gift Stanford ‘Gigy Money’
amejitangazia ushindi wa kumnasa aliyekuwa mpenzi wa Wema Sepetu, Idris
Sultan huku akitamba kuwa, sasa atamzalia mtoto.
Awali kulikuwa na vita nzito kati ya Wema na Gigy ambapo wakati Wema
akiendelea kupalilia penzi lake, Gigy aliibuka na kudai kuwa,
atahakikisha anampata Idris akiamini kuwa ndiye mwanaume wa ndoto zake.
Kufuatia vita hiyo ambayo iliibuka baada ya Gigy kunaswa na Idris usiku
wakiwa kimahaba kwenye ukumbi mmoja wa burudani uliopo Mikocheni jijini
Dar, Wema hakuonesha kujali badala yale aliendeleza msimamo wake kuwa
yeye ndiye ‘Mrs’ Idris na wengine waliokuwa wakijipendekeza hawakuwa na
chao.
Gigy ajiweka pembeni
Kufuatia Wema kukomalia penzi lake, Gigy alijishtukia na kuamua kukaa
pembeni licha ya kwamba mara kadhaa alikuwa akisema kuwa ipo siku
atatimiza ndoto yake ya kutoka na Idris.
“Mimi kwa kweli nampenda sana Idris, najua yuko na Wema lakini ipo siku
kile ninachokiwaza kitatimia,” alisema Gigy miezi kadhaa iliyopita
akionesha kuwa hatakata tamaa kupigania penzi la mshikaji huyo.
Wema, Idris watibuana
Katika kile ambacho kilionekana ni furaha kwa Gigy, hivi karibuni Idris
aliibuka na kusema kuwa, yeye na Wema wameachana na vile walivyoonekana
pamoja kwenye ile shoo ya Black Tie iliyofanyika kwenye Ukumbi wa King
Solomoni, Upanga jijini Dar mwezi uliopita ilikuwa ‘kupritendi’ tu.
Katika kuonesha kuwa kweli amefunga ukurasa wa mapenzi na Wema, Idris
alisema kuwa, siku si nyingi atamtangaza mpenzi wake mpya, jambo ambalo
lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na wengi.
Baada ya Idris kutoa tamko hilo, siku chache baadaye alionekana
akijiachia ‘kimalovee’ na Gigy ambapo alipoulizwa kama mwanadada huyo
aliyefungashia kinoma ndiye aliyechukua nafasi ya Wema, hakuwa tayari
kuongea lolote ila Gigy alipotafutwa alisema kuwa, sasa ni mwendo wa
mahaba niue.
Gigy atangaza kumzalia Idris
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Gigy alisema kuwa, Wema amechemka
katika suala la kumzalia Idris aliyekuwa na hamu ya kuitwa baba, sasa
yeye atahakikisha ndani ya siku chache zijazo anabeba mimba.
“Nilisema kwamba ipo siku ndoto yangu itatimia, Mungu kaniona na sasa
najitahidi sana nisichukue siku nyingi niwe nimembebea mimba Idris na
kumzalia mtoto.
“Unajua mimi nikimpenda mtu bwana inakuwa ni shida na lazima nimfanyie
kitu ambacho kitakuwa historia, naweza kusema nina jini mahaba ambaye
ananisumbua hivyo mkiniona kitumbo ndii, mjue ndiyo vile…” alisema Gigy.
Idris huyu hapa
Kufuatia kujigamba huko kwa Gigy, Ijumaa lilimtafuta Idris na kumuuliza
kama kweli amejiandaa kuzaa na msanii huyo ambapo kama kawaida yake
alisema ni kweli wako karibu na ukaribu wao unatokana na kwamba
wanafanya kazi pamoja katika Kituo cha Redio cha Choice FM ila hayo
mengine hataki kuyazungumzia.
Ikumbukwe kwamba, hata wakati Idris anaingia kwenye uhusiano na Wema
alikuwa mzito kukubali lakini baadaye Wema akaamua kuweka mambo
hadharani kwani mwanadada huyo si mtu wa kuwa kwenye penzi la kificho.
Friday, August 5, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment