KUELEKEA
ukingoni mwa Michuano ya kirafiki ya Kimataifa (ICC), Jioni ya leo
ndani ya dimba la Wembley jijini London, takribani watazamaji 90,000
wanadhamiwa kukaa vitini kuutazama mtanange mkali wa kukata na shoka
kati ya majogoo wa jiji Liverpool na mabingwa wa Laliga Fc Barcelona.
Mpambano huu unawakutanisha mabingwa wa Ulaya mara 5 kila moja.
Timu
hizi mbili zimewahi kukutana katika mchezo wa kirafiki kama huu
takribani miaka 40 iliyopita, zilikutana mwaka 1977 ndani ya dimba la
Olympic Stadium, Amsterdam huko Uholanzi ambapo Liverpool wakiwa chini
ya kocha Bob Paisley, walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na David
Johnson.
Baada
ya hapo timu hizi zimewahi kukutana tena mara sita katika mashindano ya
Ulaya tangu mwaka 2001-2007, ambapo kila timu iliweza kupata ushindi
mara mbili, kupoteza mara mbili na kutoka sare mara mbili.
Tarehe
5/4/2001 timu hizi zilikumbana katika michuano ya Uefa Cup, Nou Camp,
Barca wakiwa na magwiji kama Luis Enrique kocha wa sasa wa timu hiyo,
Pep Guardiola, Patrick Kluivert na Rivaldo, huku Liver ikiwa na nyota
kama Robbie Fowler, Steve Gerard na Michael Owen. Timu hizi hazikuweza
kufungana.
Tarehe
19/4/2001, kwenye Uefa Cup huko Anfield Liverpool wakapata ushindi wa
bao 1-0, bao lililofungwa na Gary McAllister. Lakini mwaka huo huo 2001
November 20 katika uwanja wa Nou Camp Barcelona wakailaza Liverpool kwa
mabao 3-1, Liver walianza kwa bao la Michael Owen lakini Barca wakapata
mabao yao kupitia kwa Kluivert, Overmass na Rochemback. 2002, March13,
kwenye Champions league huko Nou Camp timu hizi hazikuweza kufungana.
Februari
21-2007 katika michuano ya Champions League ndani ya dimba la Camp Nou
wenyeji Barcelona walilala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Liverpool kwa mabao
ya Craig Bellamy na John Arne Riise huku Deco akiifungia Barcelona bao
la kufutia machozi.
Mwisho
ilikuwa 2007, March 6, katika uwanja wa Anfield kwenye michuano ya
Champions League Liverpool ililala dhidi ya Barcelona kwa bao 1-0, goli
ambalo lilifungwa na Eidur Gudjohnsen. Wakati huo Barcelona walikuwa
wamesheheni wakali kama vile Samwel Eto'o, Ronaldinho na Lionel Messi.
Kivutio
kikubwa katika mchezo huu ni urejeo wa mchezaji Luis Suarez alijiunga
na Barcelona akitokea Liverpool huku akiwa ni kipenzi cha mashabiki wa
timu hiyo, swali ni je atapokewa vipi?
0 comments:
Post a Comment