MECHI TATU ZA KUKATA NA SHOKA KUPIGWA LEO KATIKA MICHUANO
Kwa
wapenzi na wakereketwa wa burudani ya mchezo wa gozi la ng'ombe yaani
kandanda,leo watapata burudani ya aina yake kutoka Sweden na Marekani
pale timu 6 zitakapo teremka dimbani kupambana katika mfululizo wa
michuano ya kirafiki ya kimatifa (ICC) .
Jijini
Stockholm huko Sweden mabingwa wa ligi kuu ya Hispania (LALIGA), FC
Barcelona watapambana na mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza (EPL),
Leicester City, mchezo ambao wachambuzi na wafuatiliaji wa maswala ya
kabumbu wanasema kuwa Leicester City kumfunga Barcelona ni sawa na David
kumpiga Goliath.
Barcelona
ambao kwenye mchezo wao wa kwanza waliizamisha klabu bingwa ya Uskochi
Celtic kwa mabao 3-1, huku ikiwatumia wachezaji wengi wa kikosi cha pili
(timu B) wataweza kuendeleza ubabe wao kwa kuzingatia upana wa kikosi
walicho nacho. Kwa upande wa Leicester City ambao wao katika mchezo wao
kwanza walivulumishwa mabao 4-0 kutoka PSG,watakuwa na kazi ya ziada
kuweza kupambana na kupata ushindi dhidi dhidi ya Barcelona.
Nako
huko Marekani kwenye jimbo la New Jersey jijini Rutherford ndani ya
dimba la Met Life Stadium mabingwa wa Bundesliga,ligi kuu ya Ujerumani,
watapambana na vijana kutoka Hispania, Real Madrid ambao ni mabingwa wa
Uefa.
Mchezo
huu unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na vikosi vyote
kusheheni wachezaji mahiri ndani ya dimba,Timu zote hizi zimecheza
michezo miwili miwili zikiwa zimepoteza mchezo mmoja na kushinda mchezo
mmoja. FC Bayern wao walifungwa na AC Milan ya Itali kwa mikwaju ya
penati baada ya sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 90, kisha kuifunga
timu ya Chelsea. Madrid wao walinza kwa kupoteza dhidi ya PSG,na
kuifunga Chelsea mabao 3-2.
Kocha
wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ambaye aliwahi kuifundisha Real Madrid
amesema kuwa anajivunia zaidi mchanganyiko wa damu changa na kongwe
katika kikosi chake, hvyo anategemea kupata ushindi.
Kama
hiyo haitoshi ndani ya jimbo la Minneapolis katika uwanja wa Us Bank
Stadium,timu ambazo hazikufanya vizuri kwenye ligi zao,AC Milani kutoka
(SERIE A) ligi kuu ya Italia na Chelsea (EPL) ligi kuu ya Uingereza,
zinapambana katika mfululizo wa michuano hiyo ya ICC.
Katika
michezo yao ya awali Chelsea iliifunga Liverpool bao 1-0 na baadaye
kufungwa na Real Madrid mabao 3-2 wakati AC Milan waliifunga Bayern
Munich kwa penati,kisha kupata kichapo cha mabao 2-0 toka kwa majogoo wa
jiji,Liverpool. Kocha mpya wa Chelsea Antonio Conte anategemewa
kutumumia uzoefu wake wa ligi ya Italia na kuifahamu vilivyo timu ya AC
Milan kuweza kuisambalatisha timu hiyo.
Utamu
wa michuano hii unategemewa kumalizika siku ya tarehe 8/8/2016 kwenye
dimba la Wembely,jijini London kati ya Liverpool na Barcelona.
0 comments:
Post a Comment