Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta akiwatibua baadhi
ya ndugu zake huku wengine wakimuita mchafu kutokana na kitendo cha
kumpachika mimba mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ kisha kuwepo madai
kuwa ‘amewajaza’ pia mamodo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ na Irene Hilary
‘Lynn’.
Mmoja wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake
alisema kuwa, familia imeshtushwa na madai kuwa kijana wao huyo mbali na
kwamba Zari a.k.a Mama Tiffah ni mjamzito, amewapa mimba tena Mobeto na
Lynn.
ILIKUWAJE?
Miezi kadhaa nyuma, yaliibuka madai kuwa Zari ni mjamzito lakini Diamond
amekuwa mgumu kulizungumzia hilo licha ya hivi karibuni mazazi mwenziye
huyo kutundika picha akionesha kitumbo chake kilichodhihirisha kuwa
ndani yake kuna kiumbe.
LYNN NAYE
Huku mashabiki wa Zari ‘Team Zari’ wakionesha furaha ya staa wao
‘kumshika’ mwanamuziki huyo kwa kumbebea ujauzito mwingine, zikaibuka
taarifa nyingine kuwa, modo wa Wasafi Classic Baby (WCB) Lynn naye ana
mimba ya jamaa huyo.
Ikadaiwa kuwa, kubeba ujauzito kwa Lynn kumekuja baada ya yeye na
Diamond kuwa kwenye uhusiano wa siri huku mama Diamond, Sanura Kassim
‘Sandra’ akidaiwa kujua kila kitu na kubariki ujio wa mjukuu mwingine.
MIMBA YA MOBETO
Katika kile kilichoonesha kuwachefua baadhi ya wanandugu, hivi karibuni
yakaibuka madai kuwa, mwanamitindo Mobeto naye ana mimba na mhusika ni
baba Tiffah.
Taarifa hizo zimeonesha kuwashitua wengi akiwemo mama mzazi wa modo
huyo, Shufaa Lutigunga ambaye alipoongea na mwandishi wetu alisema kuwa,
amezishangaa ila anayeweza kueleza ukweli ni Mobeto.
Jitihada za kumpata modo huyo ili kuzungumzia madai hayo hazikuzaa
matunda licha ya kwamba aliwahi kuongea na gazeti hili na kukanusha
madai yaliyokuwa yamezagaa kuwa anatoka na Diamond.
FAMILIA YA DIAMOND ‘YAMAINDI’
Kufuatia madai hayo, ndugu wa karibu wa Diamond aliyeongea na gazeti
hili alisema kuwa, hivi karibuni familia ilikaa kikao kujadili mambo ya
kifamilia lakini pia wakaonesha kukasirishwa na taarifa ya Diamond
kuwapachika mimba wasichana watatu.
“Hilo la madai kuwa Diamond amewapa mimba wanawake watatu licha ya
kwamba hatuna uhakika nazo, zimetuchefua sana, zimetufanya tumuone
Diamond ni mchafu au kwa maana nyingine ni mchafuzi.
“Nasema hivi kwa sababu, haiwezekani iwe amempa mimba Zari halafu wakati
huohuo awe amempa tena Lynn na Mobeto, sisi kama familia tutaficha wapi
nyuso zetu wakijifungua?
“Ishu hiyo imemfanya kila mtu kwenye familia awe muoga, kwani pamoja na
hayo yote kutokea, kubwa wanalohofia ni namna watakavyomwangalia Zari
(wifi yao), sasa wakijifungua sijui watamjibu nini au wataweka wapi sura
zao.
“Hapa ninavyokwambia mama Diamond na Esma hawaongei vizuri na Zari
kufuatia kuendelea kuwahisi wao ndiyo kikwazo kikubwa cha kumuunganisha
Diamond na warembo hao,” kilidai chanzo hicho.
DIAMOND HUYU HAPA
Gazeti hili baada ya kupenyezewa taarifa hizo lilimtafuta Diamond ili
kumpa nafasi ya kulizungumzia kinagaubaga suala hilo, alipopatikana
alisema kwamba yote yanayozungumzwa ni maneno ya watu na hakuna hata
moja la kweli.
“Hakuna hata moja la ukweli, mwenyewe najionea kwenye mitandao kama
nyinyi, kwani ‘social network’ kila mmoja ana uhuru wake wa kuongea
anachokiwaza na siwezi kuwafuata na kuwauliza.
“Kwa hilo sina la kuongea zaidi maana naona ni mambo ya kipuuzi tu
ambayo siwezi kuyapatia nafasi yoyote kwangu, naona tuachane nayo tu,”
alisema Diamond.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Diomond amekuwa na skendo kibao za ku-date na wasichana mbalimbali
wakiwemo mastaa ambapo mbali na Zari, Mobeto na Lyn, jamaa huyo aliwahi
pia kutoka na Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Jacqueline Wolper, Upendo
Mushi, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Aunt Ezekiel na wengineo.
Thursday, August 4, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment