Thursday, August 4, 2016

11:12 PM
Ni muendelezo wa good news kwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta kuwa sehemu ya kikosi cha KRC Genk kilichoisaidia timu kupata matokeo ugenini dhidi ya wenyeji wao Cork City.

Katika mchezo huo wa pili wa round ya pili KRC Genk wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya wenyeji wao Cork City ya Ireland, mchezo huo ambao umechezwa katika uwanja wa Turners Cross nchini Ireland, umekuwa ni furaha kwa watanzania kuona Samatta anaelekea kutimiza lengo lake la kucheza hatua ya Makundi ya michuano ya Europa League.

0 comments:

Post a Comment