Vijana
waliovyalia jezi za nyumbani na ugenini za timu ya Simba kwa msimu wa
ligi ya Vodacom Tanzania bara 2016/17 wakizinesha jezi hizo wakati wa
hafla iliyoandaliwa na wadhamini wakuu ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali
kwa timu zitakazoshiriki ligi hiyo.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko
na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura(kulia)
Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi
Mwiyombella(mwenye miwani)na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,
Boniface Wambura wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa klabu
mbalimbali wakati wa hafla ya ukabidhi vifaa kwa timu za ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi hiyo
jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi
Mwiyombella akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu
zitakazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Jijini Dar es Salaam
leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura akitoa neno la
shukurani kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zitakazoshiriki ligi
kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Hafla hiyo iliandaliwa na wadhamini wakuu
wa ligi hiyo Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
TIMU
zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Zimekabidhiwa vifaa
mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania, Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki
ligi hiyo vina thamani ya shilingi milioni 514,208,400 /=.
Akikabidhi
vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa kampuni hiyo,Nandi Mwiyombella ,alisema kuwa kwa mara
nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri
Vodacom inakabidhi vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi
mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za
mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika.
“Tunajisikia
furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza matakwa
ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi
zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi wa 2016/2017”Alisema
Mwiyombella.
Mwiyombella
alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo
unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda
kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya
mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa
duniani kote,ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na
taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.
Aliwataka
wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na
kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha
nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu
kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi
kwa kuwa vipaji vinaanzia ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na
kuendelezwa ”Alisema Mwiyombella.
Naye
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,Boniface Wambura aliishukuru hiyo,
na kuzitaka klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuheshimu chapa ya mdhamini
wakati wote wa mechi za ligi.
“Ninatoa
mwito kwa klabu zote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini mkuu katika
kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”alisema.
Aliongeza
kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu
inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini
kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema
ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika
mapema pia timu zitazoshiriki zimejiandaa vya kutosha kuhakikisha ligi
inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.
0 comments:
Post a Comment